Home » Name » Blandina Chagula

Blandina Chagula

Nickname: 
Johari
Date of Birth: 
Saturday, July 23, 1983
Place of Birth: 

Biography

Early life Johari amezaliwa amezaliwa tar. 28 Julai, 1983 mkoani Shinyanga, kupata elimu yake ya msingi huko huko mkoani shinyanga katika shule moja inayoitwa bugoyi alipohitimu mwaka 1996, na baadae kupata elimu yake ya sekondari katika shule moja inayoitwa buluba huko huku Shinyanga kabla ya kuja kumalizia elimu yake hiyo kwenye shule ya greens iliyoko jijini Dar es salaam. Baada ya kumaliza kidato cha nne alisomea mambo ya “secretariat” na baadaye alisomea mambo ya hoteli hapa hapa jijini Dar es saaam Career Baada ya kumaliza kidato cha nne alisomea mambo ya “secretariat” na baadaye alisomea mambo ya hoteli hapa hapa jijini Dar es saaam Johari anasema alianza kujiingiza kwenye mambo ya sanaa toka alipokuwa mdogo na anasema alianza kuigiza toka akiwa shule ya msingi na na kanisani kwani ni kitu alichokuwa anakipenda tokea akiwa mdogo sana Johari alianza kuigiza rasmi kupitia kundi la kaole, na anasema kuwa alienda mara ya kwanza kwenye kundi hili na akaomba fomu ya kujiunga nalo na kuanza kufanya mazoezi ya kuigiza. Anukumbuka kuwa ilimchukua muda wa mwaka mzima akifanya mazoezi na kundi hili kabla ya kupata nafasi ya kuigiza rasmi kwenye luninga. Akiwa kaole ndipo nyota yake ilipoanza kung’aa kwani baada ya kuigiza kwa muda mrefu kwenye kundi hili ndipo alipokutana na marehemu Steven Kanumba na Vicent kigosi (Ray) na kuanza mchakato wa kuanza kuigiza filamu tofauti na tamthilia walizokuwa wanafanya baada ya msukumo mkuba toka kwa marehemu Steven kanumba kuwa inabidi wabadilike na kuanza kufanya vitu vya kisasa zaidi. Baada ya hapo akiwa na Steven Kanumba na Vicenti Kigosi (Ray) walipata mdhamini wa kuwawezesha kuigiza filamu yao ya kwanza (Kampuni ya Mtitu Game) iliyoitwa Johari ambayo anasema wazo lake lilitokana na igizo lao la tufani lililokuwa likioneshwa na kituo cha television cha ITV kipindi hicho. Baada ya filamu hiyo kuingia sokoni iliwapa moyo na wakaamua kuachana a maigizo na kujikita zaidi kwenye filamu. Johari ni mmoja wa waigizaji waliofanya filamu nyingi sana hapa na nchini na anasema kuwa ameshafanya zaidi ya filamu thelathini (30) Kwa sasa anamiliki kwa pamoja na Vicenti kigosi kampuni ya utengenezaji filamu ya RJ company yenye makao makuu yake maeneo ya sinza jijini Dar es salaam. Akizungumzia mafanikio yake katika filamu Johari amasema kuwa kwa sasa angalau kuna matunda kidogo yanayotokana na uigizaji filamu ila bado anaamini kuwa kuna mambo makubwa zaidi yanaweza kufanyika katika kukuza tasnia yetu hii ya filamu hapa nchini ili iweze kuwanufaisha watu wengi zaidi.

Director

9765

Add your comment