Home » News » Baada ya ‘Black Panther’ Lupita Nyong’o anakuja tena kwenye hii

Baada ya ‘Black Panther’ Lupita Nyong’o anakuja tena kwenye hii

Leo February 26, 2018 Baada ya kufanikiwa kuigiza filamu inayofanya vizuri kwa sasa ya ‘Black Panther’, Muigizaji Staa Lupita Nyong’o ametangaza kuwa ataigiza kwenye filamu mpya na mchekeshaji na mtangazaji wa runinga wa Afrika Kusini Trevor Noah.

Lupita ataigiza kama Mama yake Trevor kwenye filamu hiyo ambayo itaigwa kutoka kwenye kitabu cha Trevor Noah cha ‘Born A Crime’. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lupita ametangaza kushiriki katika Filamu.

“Niliposoma kitabu cha @TrevorNoah cha ‘Born A Crime’, sikuweza kukiweka chini. Nina furaha kutangaza kuwa nitashiriki kuigiza filamu iliyoigwa kutoka kwa kitabu hicho! #BornACrime.” 

Kwa sasa, Lupita anafanya Promotion ya Filamu aliyoshiriki hivi majuzi ya ‘Black Panther’ iliyowashirikisha waigizaji Waafrika. 

Kitabu cha ‘BornACrime’ kilichapishwa mwaka wa 2016 na kinazungumzia maisha ya utotoni ya Trevor baada ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. 

Kitabu hicho kwenye sehemu moja kinaeleza jinsi Mama yake mchekeshaji huyo alivyomtupa nje ya gari alipodhania kuwa dereva wa gari walimokuwa ndani ambaye alikuwa wa kabila lingine alijaribu kuwauwa. Trevor anapatikana baadaye akiiba gari eneo fulani Afrika Kusini.

 

Source: MillardAyo

Add your comment