Home » News » MAN WATER!! WASAFI KUTOA NGOMA BAADA YA ALIKIBA: “…lazima itapotea”

MAN WATER!! WASAFI KUTOA NGOMA BAADA YA ALIKIBA: “…lazima itapotea”

August 25, 2017 mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba aliachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Seduce Me’ ambao umekuwa gumzo ambapo saa chache baadaye WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz waliachia video yao mpya pia ‘Zilipendwa’ kitendo kilichopokelewa kwa hisia tofauti.

Mmoja wa watu waliopokea tofauti ni pamoja na Producer wa ‘Seduce Me’ Man Water ambaye amekaa na Ayo TV na millardayo.com ambapo pamoja na mambo mengine imezungumzia ishu hiyo akisema lazima wasanii wanapoachia nyimbo zao lazima wapeane nafasi na kama wimbo uliotoka baada ya Alikiba basi hautadumu kwenye soko, utapotea.

>>>”Wasanii ufike wakati tusifanye kwa ushindani – kama upande mmoja umeshaachia wapeane nafasi kama tunataka kujenga na kutengeneza hits vinginevyo tusipoangalia tutauwa tunaziua na wasanii watapotea kwa haraka sana kwa sababu hazitokuwa kazi zaubunifu bali za kupanic.

“Kama kuna ngoma imetoka katika hali ya ushindani, nina uhakika kwamba asilimia kubwa itapotea. Siitabirii vibaya ila kuna mambo ya kujipanga ili kupeana nafasi.” – Man Water.

Source:MillardAyo

Add your comment