Home » News » Maneno ya Shyrose Bhanji kuhusu ujumbe katika Akaunti yake ya Instagram

Maneno ya Shyrose Bhanji kuhusu ujumbe katika Akaunti yake ya Instagram

Usiku wa February 25, 2018 katika ukurasa wa Instagram wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji, uliandikwa ujumbe unaosema “Sikubaliani na utawala wa Rais JPM…Niko tayari kwenda jela.”

Hata hivyo asubuhi ya leo February 26, 2018 Shyrose kupitia ukurasa wake huo huo wa Instagram ameandika kuwa hakuwa yeye aliyeweka ujumbe ule wa jana usiku kuhusu Rais John Magufuli bali akaunti yake ilidukuliwa.

Kwenye post hiyo ameandika “Account yangu ya Instagram ilikuwa hacked na watu wasiojulikana ambao walipost vitu ambavyo sihusiki navyo. Naomba radhi kwa Rais wangu JPM na wote waliokerwa na jambo hilo.” 

Add your comment